USHAIRI

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali:

Hakika siku ya leo, ni siku ya majivuno
Basi pasiwe na choyo, na usonono
Tulekezane yaliyo, unawiri Muungano.

Tuzisafisheni nyoyo,  pasiwe na miguguno
Yaongoke tutakayo, kusiwe na mabishano
Mbegu hii tupandayo, ilete mema mavuno.

Tufungulie upeo, Mola usiye mfano
Pa kitasa na komeo, tupite bila kinzano
Tupitishe njia hiyo, pasina masongamano

Twakuomba uumbao, mkono vyanda vitano
Tushikane hii leo, tuwe moja tangamano
Tupendane kwa pumbao, hali na maridhiano

Aliye ana machukiyo, adui wa Muungano
Naazibe masikiyo, asisikie maneno
Kisha awe kibogoyo, asiwe na moja jino.

Ya Ilahi ujalie, juu wetu Muungano
Nuru yake izagae, na nguvu za mapigano
Hasidi mpe hakie, mateso yaso mfano

Watamati komeleo, kuimba kwangu hukuno
Nataka maendeleo, yasiyo na malumbano
Daima tuwe ni ngao, palipo msagurano

MASWALI

(i) Lipe shairi hili anwani yake. (alama 2)
(ii) Liweke shairi hili katika bahari mbili ukitumia:  (alama 2)
          Idadi ya
            (a)    Mishororo
            (b)    Vina
(iii) Onyesha muundo wa shairi hili. (alama 5)
(iv) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 3)
(v) Toa mifano ya idhini ya kishairi iliyotumika katika shairi hili. (alama 6)
(vi) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi. (alama 2)
    (a)    Usonono –
    (b)    Msagurano –

MAJIBU

Upgrade or Subscribe

Oops! Unlock More Access Rights:

If you find that you are not subscribed, consider upgrading your account or subscribing to the necessary plan to gain access.

Elimu Assistant Team

By Elimu Assistant Team

Get in Touch!If you need any educational resources, feel free to reach out directly. I'm here to help!Name: Mr. Atika Email: nyamotima@yahoo.com Phone: 📞 0728 450 425Let’s empower your learning journey together!

Leave a Reply