Swali
SEHEMU YA A: SHAIRI (ALAMA 20)
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Kimya changu kimezidi,navunja yangu subira,
Merejeya kwa miradi,kuhitimisha dhamira,
Kukejeli sina budi,niwafunze utu bora,
Nani aali zaidi,wakenya au vinara?
Sirikali bila hadi, ndo kiini cha madhara
Yanopiga kama radi,isokuwa na ishara,
Yamini kuwa gaidi, wakitupora mishahara,
Nani aali zaidi, Wakenya au Vinara?
Wamejifanya hasidi, wasopatana kifikira,
Wana yao maksuudi, kujizombea ujira,
Wakilenga kufaidi,tumbo zao za kichura,
Nani aali zaidi, Wakenya au Vinara?
Nchi yetu kufisidi, ni jambo linonikera,
Tangia siku za jadi, ufukara ndo king’ora,
Kutujazeni ahadi, nyie mkitia fora,
Nani aali zaidi, Wakenya au Vinara?
Maskini watozwa kodi, wapwani na walo bara
Kwa uvumba na uudi, mwa walipa kwa hasara,
Hamudhamini miradi, mejihisi masogora,
Nani aali zaidi, Wakenya au Vinara?
Mesema kazi ni chudi, basi sirikali gura,
,Nafsi zenu mzirudi,mkubali kuchakura,
Makondeni mkirudi,muondoe ufukara,
Nani aali zaidi,Wakenya au Vinara?
Ujanjenu umezidi, demokrasia bakora,
Debeni takaporudi, michirizi kwenye sura,
Kuwachuja al muradi, kwa za mkizi hasira
Nani aali zaidi,Wakenya au Vinara?
Maswali
(a)
Toa anwani mwafaka kwa shairi hili.
(ala 1)
(b) Ainisha shairi hili kwa jinsi tatu na kutoa sababu. (ala 3)
(c) Onyesha mbinu za tamathali lugha katika shairi hili. (ala 2)
(d) Bainisha matumizi matatu ya uhuru wa mshairi katika shairi hili. (ala 3)
(e) Andika ubeti wa nne katika mtindo tutumbi. (ala 4)
(f) Fafanua maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili (ala 3)
(g) Taja mpango mmoja unaotajwa kama njia ya kutatua matatizo ya nchi. (ala 1)
(h) Eleza muundo wa shairi hili. (ala 3)