Soma
shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata
KUPE
NA KUNGUNI
KUPE:
Uchokozi ni wa nini
Ewe
ndugu mkunguni?
Tu
pamoja mawindoni
Ya
nini kunihaini?
Unyonyaji
kunita?
KUNGUNI:
Kupe usinilaumu
Sisi
sote wanwa damu
Ela
moja ufahamu
Pamoja
hatutadumu
Mwisho
utaangamia
KUPE:
Uchongezi wako wewe
Tamaa
yako mwenyewe
Wataka
watu wajuwe
Mwisho
sote tuuliwe
Na
ukoo kupoteza.
KUNGUNI:
Mimi hunwa nikaenda
Bali
wewe unaganda
Hadi
kuwapa vidonda
Ndipo
tiba wameunda
Majosho
kukuoshea.
KUPE:
Japo mimi sikinai
Sitarajii
uhai
Nitakwenda
kwa mbuai
Walio
hawatambui
Yao
damu tajinwia
KUNGUNI:
Kuna wanyama wa pembe
Wendapo
wakukurumbe
Na
wale wasio pembe
Meno,kwato,vyao
vyembe
Mwilio
kupasulia.
KUPE:
Tajizika manyoyani
Ndani
ndani turabuni
Ngozi
na masikioni
Na
kwengineko laini
Katu
ha’tonifikia.
KUNGUNI:
Nakwambia zindukana
Kuna
madawa mwanana
Kuosha
na kudungana
Uhai
hutauona
Siambe
sikukwambia
KUPE:
Hapo hujasema kitu
Nami
sitaacha katu
Kuna
wanyama wa mwitu
Wasiofungwa
na watu
Dawa
hawatajitia
KUNGUNI:
Kwa vile hujaghairi
Meshika
yako hiari
Puuza
langu shauri
Mwisho
utatasawari
Hapo
tungo naishia.
MASWALI
(a)
Hili
ni shairi la aina gani? (alama
2)
(b)
Eleza
maadhui ya shairi hili
(alama
3)
(c)
Bainisha
sababu ya kutumiwa kwa maswali ya balagha
(alama
2)
(d)
Eleza
umbo la shairi hili. (alama
4)
(e)
Ni
sababu gani inayoonyesha kuwa kunguni si mchochezi.
(alama 2)
(f)
Andika
ubeti wa sita kwa lugha ya nathari.
(alama
4)
(g)
Eleza
maana ya maneno (alama
3)
(i) majosho
(ii) uchongezi
(iii) mwanana