Soma shairi lifuatalo kisha  ujibu maswali.

Hung’ atuki hubanduki

Tokea utotoni watawala

 Miaka na mikaka tumekuchoka.

Hung’atuki hubanduki

Unayofanya siyo haki

Unayofanya kiimla

Demokarsia i wapi?

 

Hung’atuki hubanduki

Mamlakani wakatalia

Kheri kupe anyonyae damu

 

Hung’atuki hubanduki

Wapinzani

Unawaangusha

Misalaba meliwa na mchwa

Ni wangapi?

Walokupinga wako wapi?

Sandani!

 

Hung’atuki hubanduki

 Nani kakutia gundi?

Wape vijana nafasi

Nguvu mpya

Tutende,tubadili sera

Tupande mbegu ya demokrasia.

 

Hung’atuki hubanduki

Umeligawanya jeshi

Wakuungao wakuheshimu

Waasi  wakusaka

Umejisetiri!

Makasri ya mawe

Yasosikika mabomu

Si Atomiki wala nuklia.

MASWALI

(a)        Utungo huu ni wa aina gani?  Thibitisha.     (alama 4)

(b)        Taja maudhui matatu yanayojitokeza katita shairi hili     (alama 3)

(c)        Thibitisha matumizi ya mishata katika shairi hili    (alama 4)

(d)       Eleza toni ya shairi hili     (alama 2)

(e)        Kwa nini nafsineni inataka kiongozi ang’atuke mamlakani?    (alama 4)

(f)        Uongozi unaoendelezwa katika shairi hili ni wa aina gani?    (alama 1)

(g)        Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili.  (alama 2)

        (i)         Wapinzani umewaangusha

        (ii)        Umejisetiri

MWONGOZO

Upgrade or Subscribe

Oops! Unlock More Access Rights:

If you find that you are not subscribed, consider upgrading your account or subscribing to the necessary plan to gain access.