Soma shairi lifuatalo kisha  ujibu maswali yanayofuata

KUPE NA KUNGUNI

KUPE:  Uchokozi ni wa nini

            Ewe ndugu mkunguni?

            Tu pamoja mawindoni

            Ya nini kunihaini?

            Unyonyaji kunita?

KUNGUNI: Kupe usinilaumu

            Sisi sote wanwa damu

            Ela moja ufahamu

            Pamoja hatutadumu

            Mwisho utaangamia

KUPE:  Uchongezi wako wewe

            Tamaa yako mwenyewe

            Wataka watu wajuwe

            Mwisho sote tuuliwe

            Na ukoo kupoteza.

KUNGUNI:  Mimi hunwa nikaenda

            Bali wewe unaganda

            Hadi kuwapa vidonda

            Ndipo tiba wameunda

            Majosho kukuoshea.

KUPE:  Japo mimi sikinai

            Sitarajii uhai

            Nitakwenda kwa mbuai

            Walio hawatambui

            Yao damu tajinwia

KUNGUNI:  Kuna wanyama wa pembe

            Wendapo wakukurumbe        

            Na wale wasio pembe

            Meno,kwato,vyao vyembe

            Mwilio kupasulia.

KUPE:  Tajizika manyoyani

            Ndani ndani turabuni

            Ngozi na masikioni

            Na kwengineko laini

            Katu ha’tonifikia.

KUNGUNI:  Nakwambia zindukana

            Kuna madawa mwanana

            Kuosha na kudungana

            Uhai hutauona

            Siambe sikukwambia

 

KUPE:  Hapo hujasema kitu

            Nami sitaacha katu

            Kuna wanyama wa mwitu

            Wasiofungwa na watu

            Dawa hawatajitia

 

KUNGUNI:  Kwa vile hujaghairi

            Meshika yako hiari

            Puuza langu shauri

            Mwisho utatasawari

            Hapo tungo naishia.

MASWALI

(a)        Hili ni shairi la aina gani?    (alama 2)

(b)        Eleza maadhui ya shairi hili          (alama 3)

(c)        Bainisha sababu ya kutumiwa kwa maswali ya balagha     (alama 2)

(d)       Eleza umbo la shairi hili.     (alama 4)

(e)        Ni sababu gani inayoonyesha kuwa kunguni si mchochezi.    (alama 2)

(f)        Andika ubeti wa sita kwa lugha ya nathari.    (alama 4)

(g)        Eleza maana ya maneno     (alama 3)

            (i)  majosho

            (ii)  uchongezi

            (iii)  mwanana

MWONGOZO

Upgrade or Subscribe

Oops! Unlock More Access Rights:

If you find that you are not subscribed, consider upgrading your account or subscribing to the necessary plan to gain access.

EUROPEAN-INVASION-AND-THE-PROCESS-OF-COLONIZATION-OF-AFRICA4.jpg

Nationalism in Mozambique: The Long Road to Independence

🇲🇿 Nationalism in Mozambique: The Long Road to Independence Mozambique was among the last African…

Kenya African National Union

Unlock Self-Assessment Test: EMERGENCE AND GROWTH OF NATIONALISM IN AFRICA

Upgrade or Subscribe Oops! Unlock More Access Rights: If you find that you are not…

Kenya African National Union

EMERGENCE AND GROWTH OF NATIONALISM IN AFRICA

🌍 EMERGENCE AND GROWTH OF NATIONALISM IN AFRICA Key Factors for the Rise of Nationalism…

Self-Assessment Test: Constitutional Changes in Kenya Leading to Independence

Self-Assessment Test: Constitutional Changes in Kenya Leading to Independence

Kenya Constitutional Changes Self-Assessment Kenya Constitutional Changes Self-Assessment Test your …

Constitutional Changes in Kenya Leading to Independence

Constitutional Changes in Kenya Leading to Independence

📜 Constitutional Changes Leading to Kenyan Independence 🇰🇪 The Journey to African Representation in …

A Comprehensive Tutorial on Female Heroes of Freedom

Women in Kenya’s Independence Struggle

👩‍💼 Women in Kenya’s Independence Struggle A Comprehensive Tutorial on Female Heroes of Freedo…

1 2 3 4 188
Elimu Assistant Team

By Elimu Assistant Team

Get in Touch!If you need any educational resources, feel free to reach out directly. I'm here to help!Name: Mr. Atika Email: nyamotima@yahoo.com Phone: 📞 0728 450 425Let’s empower your learning journey together!

Leave a Reply