Mwanafunzi Nifanye Nini?
Mwanafunzi: Mkufunzi wajiani, mtihani wazuzua?
Nikiona juu chini, jibu haliji sawia
Mwalimu waleta nini, jasho sis kututoa
Mwalimu nifanye nini, mtihani wasumbua.
Mkufunzi : Pole sana ntot’angu, lakini kazana sana
Uki taka cha mvunguni, sharti inama sana
Huruma nyingi za kwangu, hazitakupa kupona
Ni mchumia kwa jua,kivulini ala.
Mwanafunzi: Mwalimu hata ni humo, lakini mambo mzungu
Nifanye nini masomo, yakae bongoni mwangu?
Bidii ypte I mumo, nilipewa naye Mungu
Mwalimu nifanye nini, mtihani wasumbua.
Mkufunzi: Na watoto pulikeni, hamushiki mashikoni
Wakati wa masomoni, mwaporomosha yoweni
Ifike mthihani, nje meno mwatoeni
Asosikia mkuu, huvunjika mguunu.
Mwanafunzi: Mwalimu sasa ‘merudi, leo taenda kitali
Nyumbani siwezi rudi, baba ni samba mkali
Kosa langu hunirudi, mwalimu hata wavyeli
Mwalimu nifanye nini, mtihani wasumbua.
Mkufunzi: Nafasi ndiyo azizi, utyumie kwa faida
Wanaumia wazazi, pesangi kuwalipia
Fahari yao wazazi, ni watoto wengi pia.
Jina li bora sheleni, kadhalika na nyumbani.
Mwanafunzi: Ahsante sana mwalimu, masomoni takazana
Kelele ni debe mumu, kitendo husema sana
Bongo kitabu kalamu, tatumia sana sana
Walimu na wazazingu, masomoni nitapambana.
MASWALI
- Eleza hili ni shairi la aina gani?(al 2)
- Bainisha aina za urudiaji katika shairi hili (al 3)
- Eleza muundo wa shairi hili (al 3)
- Eleza huku ukitoa mfano mbinu zozote tatu za lugha zilizotumika (al 3)
- Taja na utolee mifano mitatu uhuru wa kishairi uliotumika (al 3)
- Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari (al 4)
- Taja toni ya shairi hili (al 1)
- Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi (al 1)
i) pulikani ii) kitali