Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

 Angawa mdogo, dagaa, amekomaa

Kaanga kidogo, dagaa,atakufaa

Kalia kinaya,dagaa h’ondoa njaa

 

Wa kwako udogo, kijana, sio balaa

Na sio mzigo, kijana bado wafaa

Toka kwa mtego, kijana sinyanyapaa

 

Nasaha kidogo, kijana, ukubwa jaa

Jikaze kimbogo, kijana, acha kukaa

Chimbua mhogo, kijana, usibung’aa

 

Na wake udogo,dagaa, ndani hukaa,

Kuliko vigogo, dagaa, hujambaa

Hapati kipigo,dagaa hana fazaa

 

Maisha si mwigo, kijana, ushike taa

Sihofu magego, kijana, nawe wafaa

Kazana kidogo, kijana, kugaagaa

 

MASWALI

a) Lipe shairi hili anwani mwafaka (al 2)
b) Eleza arudhi zilizofuatwa katika kutunga shairi hili (al 4)
c) Onyesha jinsi malenga alivyotumia uhuru wake (al 3)
d) Tambua bahari katika shairi hili (al 3)
e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari (al 4)
f) Tambua mbinu za lugha zilizotumika katika shairi (al 2)
g) Eleza toni ya shairi hili (al 2)

MAJIBU

Upgrade or Subscribe

Oops! Unlock More Access Rights:

If you find that you are not subscribed, consider upgrading your account or subscribing to the necessary plan to gain access.