Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Hung’ atuki hubanduki
Tokea utotoni watawala
Miaka na mikaka tumekuchoka.
Hung’atuki hubanduki
Unayofanya siyo haki
Unayofanya kiimla
Demokarsia i wapi?
Hung’atuki hubanduki
Mamlakani wakatalia
Kheri kupe anyonyae damu
Hung’atuki hubanduki
Wapinzani
Unawaangusha
Misalaba meliwa na mchwa
Ni wangapi?
Walokupinga wako wapi?
Sandani!
Hung’atuki hubanduki
Nani kakutia gundi?
Wape vijana nafasi
Nguvu mpya
Tutende,tubadili sera
Tupande mbegu ya demokrasia.
Hung’atuki hubanduki
Umeligawanya jeshi
Wakuungao wakuheshimu
Waasi wakusaka
Umejisetiri!
Makasri ya mawe
Yasosikika mabomu
Si Atomiki wala nuklia.
MASWALI
(a) Utungo huu ni wa aina gani? Thibitisha. (alama 4)
(b) Taja maudhui matatu yanayojitokeza katita shairi hili (alama 3)
(c) Thibitisha matumizi ya mishata katika shairi hili (alama 4)
(d) Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
(e) Kwa nini nafsineni inataka kiongozi ang’atuke mamlakani? (alama 4)
(f) Uongozi unaoendelezwa katika shairi hili ni wa aina gani? (alama 1)
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili. (alama 2)
(i) Wapinzani umewaangusha
(ii) Umejisetiri
MWONGOZO
Oops! Unlock More Access Rights:
If you find that you are not subscribed, consider upgrading your account or subscribing to the necessary plan to gain access.
Discover more from ELIMU ASSISTANT
Subscribe to get the latest posts sent to your email.
